4/28/2022

Mchezaji Mukoko Tonombe Anukia Azam FC


Imeelezwa kuwa kiungo wa kazi aliyewahi kucheza ndani ya Yanga, Mukoko Tonombe yupo kwenye rada za mabosi Azam FC ili kuweza kuinasa saini yake.
Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao waliweza kufanya vizuri ndani ya Yanga msimu uliopia wakati timu hiyo ilipomaliza ikiwa nafasi ya pili.

Pia alikuwa kwenye kikosi ambacho kiliweza kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho na ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Simba.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, ni bao la Taddeo Lwanga kupitia pasi ya Luis Miquissone liliweza kuipa ushindi Simba.

Habari zinaleza kuwa mabosi Azam FC wameanza mazungumzo na kiungo huyo ili kuweza kumrejesha kwa mara nyingine Tanzania.


Aliposepa ndani ya Yanga kwa makubaliano maalumu kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger