4/28/2022

Mgombea Urais Ahimiza Mabadiliko ya Jina la Nigeria Kuwa Nigritia

 


Mgombea urais wa Nigeria, Adamu Garba, anataka jina la nchi hiyo kubadilishwa na kuwa "Shirikisho la Nigriti" au kwa urahisi Nigritia.

Anasema kubadilishwa kwa jina kutakuwa sehemu ya mageuzi atakayotekeleza iwapo atashinda uchaguzi.


Uchaguzi wa rais wa Nigeria utafanyika Februari 2023. "Je, tungebadilisha jina la nchi hii, tuifanye shirikisho ipasavyo na kuibadilisha kuwa "Shirikisho la Nigriti" au kwa urahisi NIGRITIA.


Baada ya yote, Nigritia ni jina letu la zamani kabla ya Lady Lugard kuiita Nigeria," Bw Garba alitweet. "Ni wakati mwafaka wa kujisafisha kutokana na dhana mbaya, kujipanga upya na kuirejesha nchi yetu mbali na utambulisho na migawanyiko ya wakoloni kwa tafsiri zetu za umoja, utangamano, uvumilivu na mshikamano," aliongeza.


Alizitaja nchi nyingine za Kiafrika kama Ghana, Kenya, Benin na Togo ambazo zilibadilisha majina yao "yaliyochochewa na ukoloni" kuhusu uhuru, akisema kuwa "utambulisho ni kila kitu". Bw Garba pia amechapisha video inayoonyesha njia sahihi ya kutamka jina jipya lililopendekezwa

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger