Ticker

6/recent/ticker-posts

Mike Tyson Amshushia Kichapo Shabiki Ndani ya ndege

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>

Mwanamasumbwi mkongwe Mike Tyson adaiwa kupoteza utulivu kwenye ndege aliyokuwa akisafiria usiku wa jumatano Aprili 20, 2022, baada ya kuonekana akimshambualia kwa ngumi usoni, kijana aliyemsogelea akitaka ukaribu naye kupita kiasi.


Kwa mujibu wa TMZ, kisa hicho klitokea majira ya saa 10:30 usiku wakati Tyson akitarajia kuruka kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa San Francisco kuelekea Florida nchini Marekani.


Shahidi wa tukio hilo aliyekuwa kwenye ndege hiyo anasema “wakati yeye na rafiki yake wakipanda ndege ya Tyson, nguli huyo wa ndondi mwanzoni alikuwa ametulia pamoja nao na abiria wengine.”


Shahidi huyo akaendelea kwa kusema kuwa Tyson aliwakubalia kupiga picha (Selfie) na kisha akawa mvumilivu kwa dakika kadhaa mbele ya kijana huyo aliyekuwa na furaha kupita kiasi ya kuonana na Mike, kiasi cha kuendelea kujaribu kumsemesha mpiganaji huyo mwenye umri wa miaka 55 alipokuwa ameketi mbele ya kiti cha kijana huyo.


Inasemekana Tyson alikuwa na uvumilivu wa kutosha kwa kijana huyo aliyekuwa nyuma yake akizungumza kando kabisa ya sikio lake, hali iliyomfanya kushindwa kuvumilia, na ndipo Tyson alianza kurusha ngumi kadhaa usoni kwa kijana huyo.


Video inayosambaa mitandaoni inamuonyesha Tyson akimrushia mapigo mengi mtu huyo, hadi kufikia kiasi cha kumfanya avuje damu kwenye paji la uso.


Shahidi huyo anaongeza kwa kuthibtisha kuwa baada ya tukio hilo Mike alitoka kwenye ndege hiyo.


Kijana aliyepigwa ngumi alipokea matibabu na kisha akaenda polisi kuripoti tukio hilo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments