4/10/2022

Mpina akiri kumiliki ekari 700 Moro, wanakijiji wataka azirejesheMwenyekiti wa kijiji cha Dalla kata ya Mvuha Mohamed Kilimasinde (katikati) akizungumza na wananchi katika mkutano wa kawaida kijijini hapo juu ya ombi lao kwa Rais Samia Suluhu Hassan la mgogoro wa eneo la ekari 700 zinazomilikiwa na Mbunge Luhanga Mpina katika kijiji hicho. Picha Lilian Lucas.
Morogoro. Wakati wananchi wa kijiji cha Dala kata ya Mvuha mkoani Morogoro wakimwomba Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia kurejeshwa kwa ekari 700 zinazomilikiwa Mbunge wa Kisesa, Luhanga Mpina, mbunge huyo amekiri kumiliki ardhi hiyo kihalali.

Mgogoro huo ulioulianza tangu mwaka 2009 baada ya Mpina kumilikishwa ekari 300 na mkutano wa kijiji.

Alipoulizwa jana kwa simu, Mpina alikiri kumilikishwa ardhi hiyo na Serikali ya kijiji na amedai kuwa baadaye baadhi ya wajumbe wa kijiji wakajigeuza kuwa mashamba ni ya kwao.

“Hizo ekari nazimiliki kihalali na fedha kwenye akaunti niliziweka kihalali, ndio maana hata alipokwenda Mkuu wa Mkoa na Wilaya kilichokubalika ni kupima eneo.


 
“Sasa kiustaratibu katika upimaji kisheria huwezi kuingia kwenye kulipima eneo bila kukamilisha kesi iliyokuwa inaendelea,” alisema.

Wakizungumza katika mkutano wa kijiji uliofanyika jana Aprili 9, wanakijiji hao wamedai kuwa mbunge huyo amejimilikisha ardhi yao kinyume na utaratibu.

Mkazi wa kijiji hicho, Kadiri Omary akizungumza katika mkutano huo, amesema mwaka 2009 akiwa mjumbe wa Serikali ya Kijiji, Mpina aliomba kupewa hekari 300 na kupatiwa na kijiji hicho.


Amesema ilipofika 2016 Mpina aliomba kumiliki ardhi hekari 700 ili awe na ekari 1,000 ambapo mkutano mkuu wa kijiji ulikataa maombi yake na kumtaka asitumie ardhi yao.

Omary amesema lakini kutokana na mamlaka aliyokuwa nayo kwa wakati huo aliweka walinzi na kuendelea kufungua mashamba katika ardhi ya kijiji bila ridhaa ya wananckijiji.

Naye Abubakar Kiwembela walimlalamikoa kiongozi huyo bila mafanikio katika Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kwa CCM.

Amesema walilazimika kufungua shauri namba 54 la mwaka 2018 katika Baraza la Ardhi la Wilaya ambalo walishinda na kutakiwa kupatiwa eneo hilo.


 
Kama hiyo haitoshi, amesema walifungua maombi ya kukazia hukumu namba 410 ya mwaka 2022.

Maelezo hayo yameungwa mkono na mwanakijiji Idd Kibwana aliyesema kuwa, mwaka 2018 mgogoro ukiwa na miaka saba wananchi walifikisha malalamiko yao kwa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally ambaye aliwapa matumaini kwa kuahidi kushughulikia suala lao lakini halikuzaa matunda.

“Agosti 2018 Mwananchi lilichapisha kuwa Dk Bashiru kupambana na waziri anayemiliki ekari 1,000 (wakati huo Mpina alikuwa Waziri wa Mifugo na uvuvi), lakini pamoja na kauli hiyo hatukuona lolote,” amesema Kibwana.

Ameendelea kusema kuwa malalamiko hayo waliyafikisha kwa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Willium Lukuvi kupitia kikao cha Baraza la Madiwani cha Agosti 30, 2018 ambapo bado Mpina aliendelea kutumia ardhi bila ridhaa ya wananchi wala maridhiano.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mohamed Kilimasinde amekiri Serikali ya kijiji kumpa Mpina ekari 300 za awalia lizoomba mwaka 2009 lakini baada ya hapo alinyimwa ekari 700.

Amesema mwaka 2009 alifika kijiji hapo aliomba ekari 300 na kupata baada ya kujadiliwa na Serikali ya kijiji na kwenye mkutano kuu.

Amesema mwaka 2017 uongozi wa Mkoa, wilaya, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya walifika kijijini ili kufahamu hitimisho ambapo ilionekana serikali ya kijiji ilikuwa na makosa kuidhinisha ekari hizo za awali.

Kilimasinde amesema wakati huo Mpina alikuwa ameweka kwenye akaunti ya kijiji Sh35 milioni alizosema zitatumika kwa shughuli ya maendeleo.

Diwani wa kata ya Mvuha Mfaume Chanzi amesema mambo yote yaliyozungumzwa atahakikisha anayafikisha ngazi zinazohusika ili kushughulikiwa kwa haraka.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger