Mrembo Muaddi Anayesemekana Kuvunja Penzi la Rihanna Afunguka "Rihanna na Baba mtoto wake Hawajaachana"

 


Mwanadada anayetuhumiwa kujihusisha kiapenzi na Baba mtoto mtarajiwa wa Rihanna, Amina Muaddi amejibu tetesi zilizoenea mitanadaoni na kote duniani zikimshutumu kusababisha Ugomvi kati ya mwanamuziki Rihanna na rapa Asap Rocky.


Muaddi amekanusha taarifa za kuachana kati ya Asap Rocky na Rihanna, ambazo ziliripotiwa usiku wa kuamkia leo April 15, 2022 akisema tetesi hizo “asilimia milioni 1 sio za kweli.”


Katika taarifa ya Muaddi, aliyoshiriki kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta Story), mbunifu huyo aliweka bayana hisia zake kuhusu namna alivyopokea taarifa hizo zilizoibua taharuki kwa mashabiki na wadau mbali mbali kote ulimwenguni.


“Tunaishi katika jamii ambayo ni wepesi wa kuzungumza juu ya mada bila kujali msingi wa ukweli.” na kudokeza namna uzushi huo ulivyowaathiri vibaya wote watatu kwa wakati mmoja,


“Siku zote nimekuwa nikiamini kwamba uwongo usio na msingi unaoenezwa kwenye mitandao ya kijamii haustahili jibu au ufafanuzi wowote, hasa ule ambao ni mbaya sana,” ameandika Muaddi.


Muaddi ameongeza kuwa kutokana na uzito wa jambo hilo imemlazimu kujitokeza na kujibu tuhuma hizo kwa madai ya kuwa kwa sasa anahisi kulazimishwa kusema kwa sababu masuala hayo yamewahusisha watu anaowaheshimu na kuwapenda.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad