4/30/2022

Msanii Amber Lulu Amber Lulu Apewa TUZO na Youtube Kwa Hili


Mtandao wa youtube umempa tuzo (plaque) msanii Amber Lulu kwa kufikisha wafuasi (subscribers) 100,000. Amberlulu ambaye kwa sasa anatesa na ngoma yake ‘Halichachi’ akiwa amemshirikisha Kayumba, alionyesha tuzo hiyo kwa mashabiki zake jana Alhamisi Aprili 28, 2022.


Akiambatanisha picha ya tuzo hiyo ambayo ni ya silver, kwenye post yake Instagram ameandika, "Asanteni sana mashabiki wangu, asanteni youtube kwa zawadi. Ni hatua nzuri katika safari yangu ya muziki. Naomba muendelee ku-subcribe Asante."


Amber Lulu ambaye ni mzaliwa wa jijini Mbeya, alijiunga na mtandao Youtube Disemba 27, 2016 na amepata wafuasi (subscribers) wengi kutokana na kazi zake mbalimbali anazoziweka katika mtandao huo.


Amberlulu katika channel yake ya Youtube ana jumla ya video 35, zenye jumla ya views Milioni 9,713,861. Anaingia kwenye top 10 ya wanamuziki wakike Tanzania wenye wafuasi wengi katika mtandao wa youtube wakiongozwa na @officialzuchu mwenye wafuasi (subscribers) milioni 1.94

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger