Ticker

6/recent/ticker-posts

Msanii Linex Afunguka Kudhulumiwa na Msanii Rayvanny

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>


Hii leo April 29, msanii Linex alikuwa kwenye kipindi cha Empire ya EFM na moja ya ishu alizo ziongelea ni kudhulumiwa wimbo na msanii Rayvanny ,huku akikiri ni ishu ambayo hajawahi iongea popote pale na ni muda kidogo toka itokee.

Linex amedai alifanya wimbo aliomshirikisha Rayvanny, baada tu ya audio kufanyika, ilibidi arudi kujichanga pesa za kushoot video, na baada ya pesa kupatikana kuna vitu havikwenda sawa,hivyo video haikufanyika, Hali hiyo ilimlazimu Linex kupandisha Audio pekee kwenye Channel yake ya YouTube, lakini Rayvanny akaja kuishusha na baada ya muda, Linex akakuta wimbo huo upo kwenye Albamu ya Rayvanny.

Linex ni moja ya mastaa walio wahudumia mashabiki wa muziki wa Bongo Flava kwa hali ya juu sana, akifanikiwa kutengeneza hit songs kama Mama Halima,Leka Dutigite (Kigoma All Stars) Mahakama ya Mapenzi, Salima na nyingine kibao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments