Msemaji wa Simba "Iwe Mchana iwe Usiku, Mnyama Safari Hii Anaenda Nusu Fainali"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC,Ahmed Ally ameongea na Waandishi wa Habari leo kuelekea Mchezo wa Simba vs Orlando Pirates ambapo amesema safari hii Simba imedhamiria kwenda nusu fainali.

"Mchezo wetu utakuwa mchezo wa kwanza Afrika Mashariki kutumia VAR, na hili ni kwa michezo yote ya hatua ya robo fainali, kwa sasa vikao vinaendelea kwa upande wa Simba, CAF, TFF na Azam ili VAR ifanyike vizuri na tunaamini itafanya kazi kwa ufanisi"

"Mpaka sasa hatujapata taarifa rasmi kutoka Orlando Pirates kwamba watakuja lini, kesho wana mchezo kule nyumbani kwao labda baada ya mchezo watatujulisha na sisi tutawapa taarifa, kwa upande wetu kama Simba maandalizi yameshaanza, kikosi kilirudi jana kutoka Moshi, Wanasimba tusahau yaliyotokea Moshi, tunachofukuzia mbele yetu ni kikubwa kwa nchi, tarehe 17 tufanye maajabu"

"Hii ni robo fainali ya aina yake, iwe mchana iwe usiku, Mnyama safari hii anaenda semi final, tumedhamiria hilo, tumejipanga kwa hilo ndio maana tunataka mashabiki mje kwa wingi"

"CAF wameturuhusu kuingiza mashabiki 60,000, ni Simba pekee imeruhusiwa kuingiza mashabiki idadi hiyo, ni kutokana na heshima ambayo CAF wametupa, CAF wanaamini hii ni mechi kubwa ambayo kila shabiki wa mpira atahitaji kuingia uwanjani."
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad