4/23/2022

Mteja Aliyeuziwa Simu ya Iphone Bila Chaja Kulipwa Fidia ya Mamilioni na Apple

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA


Jaji Vanderlei Caires Pinheiro wa nchini Brazili ameamuru kampuni ya Apple kumlipa mteja Dola $1,081 [Tsh 2,510,082.01] baada ya mteja wao kulalamika kuwa amenunua iPhone na hapakuwa na Charger 'Adapter' kwaajili ya Kuchaji simu hio kwenye Box.
-
Kwa mujibu wa Daily Mail, Jaji ameiagiza Apple kumlipa mteja kama hasara na fidia baada kuuziwa simu na kufanya kazi ya ziada ya kutafuta charger ya simu hio. Apple wamepewa siku 10 za kutii amri ya mahakama au adhabu itaongezeka na kuwa zaidi ya dola 2000 USD.
-
Apple inakisiwa kuuza iPhone milioni 190 duniani kote tangu hatua hiyo ya kutoweka Adapter kuanza, ni hatua kubwa iliyoshangiliwa na wanamazingira ila jaji Caires amesema "Sio sahihi kwamba hatua kama hiyo inalenga kupunguza madhara kwa mazingira wakati ushahidi unaonyesha kuwa Apple wanaendelea kutengeneza kifaa hicho na kukiuza kivyake.
#SamMisagoTV
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger