4/19/2022

Mtoto Awarudisha Pamoja Rayvanny na Fahyma..Paula Alie tu Hana Chake


Drama za wazazi wenza, Rayvanny au Chui ambaye ni staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania na mwanamitindo Fahyma hazijawahi kuisha pamoja na kwamba jamaa huyo alihamishia majeshi kwa Paula Kajala.

Wengi wanavyojua na kufahamu ni kwamba Rayvanny na Fahyma walitengana kwa sababu moja ua nyingine ikiwemo skendo ya usaliti kati yao.

Baada ya kutengana kwao Rayvanny aliendelea na maisha yake huku akianzisha uhusiano wa kimapenzi na Paula Kajala.

Uhusiano wa wawili hao ulikejeliwa na wengi, huku lawama ikimwendea Paula kwani wengi walidai kwamba alivunja familia ya Rayvanny na Fahyma.

Jumamosi iliyopita Aprili 16, 2022 ilikuwa ni siku ambayo mtoto wao, Jaydanny alikuwa na kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa. Kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu, mtoto huyo amesababisha kunoga kwa wazazi wake hao wakiwa pamoja na kuoneshana mahaba mbele ya mtoto wao.

Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi kama wamerudiana, lakini hata kama hujui kusoma, video za tukio hilo zinaonesha namna ambayo wawili hao bado wanapendana.

Rayvanny aliachana na Fahyma kitambo, lakini tetesi zimeendelea kuenea kwamba wamerudiana huku Paula akidaiwa kuachwa solemba.

Kutengana kwao hakujawazuia wawili hao kumsherehekea mtoto wao ambaye wamempa jina la Chuo Mdogo. Cc; @sifaelpaul

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger