Mtuhumiwa wa Shambulio la Raia kwenye Kituo cha Treni Jijini New York, Afahamika

 


HIVI karibuni limetokea shambulio katika stesheni moja ya treni jijini NewYork nchini marekani ambapo idadi ya watu Zaidi ya 17 wamejeruhiwa na wengine wawili wakiwa mahututi.

Chanzo cha shambulio hilo ni mwanaume mmoja ambaye hakufahamika aliporusha mabomu ya machozi na kusababisha moshi mkubwa eneo la stesheni kisha kuanza kufyatua risasi akiwalenga abiria ambao walikuwa kituoni hapo kwa ajili ya huduma usafiri.

Kamishna wa Polisi wa Jiji la New York Keechant Sewell alisema:

“Mtu aliyekuwa amevaa kitambaa maalum cha kujificha sura alirusha bomu la machozi lililozua moshi mzito kisha akaanza kumimina risasi kwa abiria.”

Taarifa zilizopatikana leo asubuhi ni kwamba mtu huyo amefahamika na ni mkazi wa Philadelphia anayeitwa Frank R James (62), ambaye aliazima gari maeneo ya Philadelphia na kuja kutekeleza azimio hilo kisha kulitelekeza gari hilo.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi walikuta ufunguo wa gari, vilipuzi, bunduki aina ya Glock 9-Milimita, magazeti matatu pamoja na vimiminika ambavyo vinaaminika kuwa ni mafuta ya petrol.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi ni kwamba James aliweka baadhi ya video za tukio hilo katika mtandao wa kijamii wa Youtube zikiwa na maudhui ya kuwalaumu wanawake weusi kusababisha vurugu kwenye jamii ya watu weusi lakini pia akishutumu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kama sababu ya kuwafanya watu weupe waonekana ni watekelezaji wa mauaji ya halaiki.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad