4/27/2022

Muna Love Afunguka Mapya Baada ya Kupotea Lokesheni

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA


Muna love ni muigizaji wa kitambo wa Bongo Movies, lakini hajaonekana lokesheni muda mrefu huku akijitanabaisha kuwa ni mtumishi wa Mungu ambaye anasema hajali chuki za watu kwa sababu Mungu anamjua huku akifunguka juu ya tetesi za muda mrefu kuwa yeye ndiye alimuua (kumtoa kafara) mwanawe, Patrick ili awe tajiri.


Muna ambaye hivi karibuni alitrendi baada ya kufanya upasuaji wa viungo mbalimbali vya mwili wake ili awe supa, anasema; “Kuna wakati mtu anaweza kuniona kama chizi ila Mungu ananielewa kwakuwa ananijua na pia anajua patano langu mimi na yeye so na-focus na Mungu wangu.


“Hakuna binadamu asiyekosea huku duniani hata watumishi wa Mungu wanakosea kwakuwa ni binadamu tu, lakini Mungu anawainua tena ili kutulisha neno. “Mimi huyu hata kama hunipendi, unanichukia tu au vile unavyoamini kwa kusikia habari yangu na kujivalisha chuki juu yangu namuomba Mungu akusamehe, akujaze baraka, uishi maisha marefu ili unione mimi kama ushuhuda wako na siku moja utashuhudia popote.


“Hilo suala la kukomenti kila siku kuwa mimi nimemuua mwanangu, sasa hivi nakula raha, sina muda wa kujielezea, Mungu ananijua na unayeamini, amini tu na msidhani ndiyo fimbo ya kunirudisha nyuma nilie, machozi sasa basi. “Mimi ni ushuhuda unaoishi, mapito yangu mengi yalipita mbele yenu na hata baadhi mlijua sitaishi, nitakufa, ila kuna muweza wa yote aliye hai alinikumbatia huyu ni Yesu.


“Najivunia Yesu kunitumia, kuniadhibu, kunisamehe na kunilinda na kunishindia vita zangu. Ninatamani siku moja na wewe uwe na kitu kinaitwa imani, neno dogo ila ni mwisho wa matatizo…”


Patrick alifariki dunia mwaka 2018 baada ya kuugua kwa muda mrefu.


Mungu aendelee kuilaza roho yake mahali pema peponi!

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger