4/20/2022

Mwanariadha wa Kike Kenya Amepatikana Ameuawa Kwa Kisu


Mwanariadha wa kike amepatikana ameuawa huko Iten – mji wa Kenya ambapo mwanariadha Mwingine wa Olimpiki, Agnes Tirop, aliuawa miezi sita iliyopita – polisi wanasema.

Damaris Muthee Mutua, ambaye alizaliwa nchini Kenya lakini alikuwa na uraia wa Bahrain, alikuwa na umri wa miaka 28.

Maafisa wanasema aliuuawa kwa kudungwa kisu. Wanamsaka mpenzi wake, mwanariadha wa Ethiopia ambaye polisi wanasema ni mshukiwa mkuu.

Iten ni kambi ya mafunzo kwa wakimbiaji wa masafa marefu. Mwezi Oktoba mwaka jana mauaji ya mwanariadha Agnes Tirop yalishtua nchi.

Inaelezwa kuwa Mumewe bado yuko kizuizini na anakanusha kuhusika na mauaji hayo.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger