4/29/2022

Mzungu Ampiga Risasi Mwanamke Mweusi Baada ya Kuzani ni Kiboko


Vyombo vya Habari nchini Afrika Kusini vimeripoti kuwa Mzungu mmoja nchini Afrika Kusini aitwaye Paul Hendrik van Zyl (77), amefikishwa Mahakamani kwa kumpiga risasi na kumjeruhi Mwanamke mweusi anayedai kuwa alimdhania ni kiboko.

Mzungu huyo alikamatwa siku ya Jumanne baada ya kupiga risasi kuelekea kwa Mwanamke huyo, Ramokone Linah, ambaye alikuwa akivua samaki na mpenzi wake mtoni katika mji wa Lephalale, kaskazini mwa jimbo la Limpopo, Van Zyl anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuua, kulingana na Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka lakini yeye anajitetea kwamba alikuwa akiwapiga risasi wanyama.

Linah (38) alipata majeraha ya risasi kwenye mkono wake, wakati mpenzi wake aliyekuwa nae pamoja alifanikiwa kujificha kabla ya kutoa taarifa kwa polisi na huduma za dharura.

Mshtakiwa ndiye mmiliki wa shamba ambalo tukio hilo lilitokea na Polisi wamesema walipata bunduki kadhaa wakati wa kumkamata mshukiwa.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger