4/15/2022

Nahreel Ajibu Navykenzo Kupotezwa Baada ya Kufanya Collabo na Diamond Platnumz


Kundi la muziki Bongo, Navy Kenzo limeonyesha kupuuzia madai kuwa wamepotea tangu kuachia kolabo yao na Diamond Platnumz, wimbo "Katika".

Memba wa kundi hilo, msanii @nahreel amepangua shuti hilo kutoka kwa shabiki mmoja ambaye aliacha komenti kwenye ukurasa wa instagram wa Nahreel, kwa kuandika; "Diamond mbaya sana toka mfanye naye wimbo dah, hamsikiki naumia sana", Nahreel alimjibu shabiki huyo kwa kumuandikia; "Kaa mkao wa kula".

"Katika" ni kolabo iliyowakutanisha Navy Kenzo na Diamond Platnumz, ilitoka mwaka 2018.

Fahamu, Navy Kenzo kwasasa wanajiandaa kuachia album yao ya NNE baada ya kuachia Hold Me Back (2015), AIM - Above Inna Minute (2017) na Story Of The African Mob (2020).

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger