4/20/2022

Ndege ya RwandAir yateleza na kupoteza mwelekea ikitua uwanja wa Entebbe UgandaNdege ya abiria iliteleza na kutoka kwenye njia yake ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda Jumatano asubuhi.


Katika taarifa, RwandAir ilisema tukio hilo “lilitokana na hali mbaya ya hewa”.

Abiria wote na wafanyakazi wa ndege walishuka salama bila majeraha yoyote, iliongeza.

Mdhibiti wa anga alisema njia mbadala ya ndege kurukia inafanya kazi kwa ajili ya ndege ndogo na nyepesi.


 
“Juhudi zote zinaendelea ili kuondoa ndege kwenye ukanda wa kuruka na kutua ndege ili njia kuu ya kuruka na kutua ndege irudi kutumika kikamilifu,” ilisema.

Gazeti la Daily Monitor nchini Uganda, limeripoti kuwa abiria 20 kati ya 60 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wameratibiwa kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba.

Inaripoti kuwa tafrija ya kuzaliwa kwa Jenerali Kainerugaba ya kutimiza miaka 48 imepangiwa kufanyika Jumapili.

Jenerali Kainerugaba, ambaye pia ni kamanda wa majeshi ya nchi kavu, alichapisha ujumbe mtandaoni siku ya Jumatatu kwamba aliyekuwa Miss Rwanda atakuwa miongoni mwa wageni watakaohudhuria hafla hiyo.

Chanzo BBC.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger