4/21/2022

Pablo Amsaka Morrison Mpya SimbaKOCHA Pablo Franco ameanza kujiandaa mapema kuziba pengo la mshambuliaji wake Benard Morrison katika mchezo wao ujao wa robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates.

KOCHA Pablo Franco ameanza kujiandaa mapema kuziba pengo la mshambuliaji wake Benard Morrison katika mchezo wao ujao wa robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates.

Morrison hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano kwa sababu haruhusiwi kuingia nchini humo.
Simba kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Orlando Pirates walishinda bao 1-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa wikiendi iliyopita.

Baada ya mchezo huo jana Jumanne wachezaji wa Simba walirejea mazoezini katika uwanja wa Mo Simba Arena wakijiandaa na mechi hiyo ya marudiano na ndipo Pablo alipoweka nguvu zaidi ya kutafuta mbadala wa Morrison mapema.

Pablo alianza kwa kuwapanga wachezaji wake wote na kuwataka wacheze kwa kuutanua uwanja na kuugusa mpira mara moja.
Zoezi hilo lilifanywa kwa takribani dakika 20 baada ya hapo aliwapumzishwa wachezaji takribani wote ambao walicheza mchezo uliopita.

Pablo aliwaweka pembeni Jonas Mkude, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Pascal Wawa, Henock Inonga na Peter Banda. Wengine ni Aishi Manula, Pape Ousmane Sakho, Benard Morrison na Cris Mugalu.
Baada ya kuwaweka chini mastaa hao, Pablo akisaidiana na msaidizi wake Seleman Matola alipanga wachezaji kwa makundi mawili na kuweka uwanja nusu ili wacheze.
Pablo upande mmoja aliwapanga Lary Bwalya, Tadeo Lwanga, Clatous Chama, Kibu Denis, Jimmyson Mwanuke, Yusuph Mhilu na Mzamiru Yassin.

Upande mwingine aliwapanga Sadio Kanoute, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Israel Mwenda, Kennedy Juma na Joash Onyango.
Kwenye zoezi hilo pablo aliwataka zaidi kundi la kina Bwalya ambalo lilikuwa na viungo wengi wawe wepesi katika kupeleka mashambulizi.

Pablo alionyesha kuwakomalia zaidi Bwalya, Kibu na Mhilu hali iliyoonyesha kuwa ana mipango nao kwenye mchezo ujao.
Kocha huyo alikuwa anawasisitiza zaidi wachezaji hao wawe na uharaka kupambana na mabeki na macho yao yawe kwenye goli wanapokuwa na uwepesi wa kufanya hivyo

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger