Ticker

6/recent/ticker-posts

Pablo Anena Ushindi Dhidi ya Orlando Kisha Aguna "Tumejiweka Pazuri ila Kwao mmh"

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>

 


Kocha Mkuu Pablo Franco, ameweka wazi furaha yake ya ushindi wa bao moja nyumbani waliopata dhidi Orlando Pirates akisema unampa faida kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo nchini Afrika Kusini.


Pablo amesema michuano ya Afrika ni migumu hivyo unapaswa kutumia vema uwanja wa nyumbani ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye mchezo wa marudiano.


Pablo ameongeza kuwa wanatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Orlando kwenye mchezo wa marudiano lakini wamejipanga kuhakikisha wanaenda kufanya vizuri ugenini.


Pablo amekiri kuwa hawakuwa na matokeo mazuri kwenye mechi za ugenini katika hatua ya makundi kwa hiyo wanapaswa kujipanga hasa kutokana na ubora wa wapinzani.


“Michuano ya Afrika mara nyingi timu zinafanya vizuri nyumbani kama tulivyofanya. Tutajipanga kuelekea mchezo wa marudiano ugenini tunahitaji kufuzu nusu fainali,” amesema Pablo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments