4/16/2022

Paula: Tunatumia Helikopta Kwenda Sokoni, Awaonya Wenye Makasiriko Kukaa Kimya


Staa wa bongo muvi Frida Kajala akiwa na mwanaye Paula Paul
KAMA wewe ni mfuatiliaji wa Bongo Movies utakuwa unamjua Kajala Masanja au Frida Kajala na kama ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii utakuwa umesikia jina la Paula Kajala.

Paula Kajala ni binti wa Kajala au Mama Pau ambapo wawili hao wamekuwa wakitrendi kwenye mitandao ya kijamii; Kajala anaombwa kurudiana na Harmonize ilihali penzi la Paula na Rayvanny linadaiwa kuyumba.

Kajala na Paula ni mama na bintiye ambao wamekuwa wakieleza namna  ambavyo kwa pamoja wana ndoto ya kuja kuishi maisha ya kifahari.

Sasa bana, Paula ameshea picha zake na mama yake wakiwa wameshuka kwenye  na kusema wanatumia helikopta kuendea sokoni huko Dubai.

Paula ameonya wenye makasiriko akiwaambia wanyamaze kwani hawawezi kufikia maisha anayoishi. Paula ameposti picha hizo na kuandika;

“Yaani mimi na mama’ngu Kajala Frida tuna helikopta special ya kutupeleka sokoni Dubai, halafu anatokea tu kiswaswadu mmoja anaanza kunichamba hiyo unapata wapi hizo nguvu mbona uhuru unapitiliza, hebu nisaidieni kushangaa…”

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger