4/11/2022

Polisi Nchini Uingereza Wanamchunguza Christiano Ronaldo Baada ya Kuvunja Simu ya Shabiki


Polisi nchini Uingereza wanachunguza madai ya shambulio baada ya mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo kuonekana akivunja simu ya shabiki mmoja.

Picha zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na maoni yaliyodai kuwa alivunja simu hiyo alipokuwa akitoka nje ya uwanja baada ya timu yake kupoteza mechi dhidi ya Everton 1-0. Ronaldo baadaye aliomba msamaha baada ya video inayomuonyesha akivunja simu ya shabiki huyo kuibuka.
-
"Si rahisi kukabiliana na mihemko katika nyakati ngumu kama ile inayotukabili. Ningependa kuomba radhi kwa hasira yangu na, ikiwezekana, ningependa kumwalika shabiki huyu kutazama mchezo huko Old Trafford kama ishara ya mchezo wa haki na uanamichezo.” alisema Ronaldo.

Chanzo: bbcswahili

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger