4/13/2022

Poshy Qeen Atamba "Kujifungua Kumenifanya Niwe Mrembo Zaidi"


MWANAMAMA ambaye alipata umaarufu kutokana na umbo lake matata la nyingu kwenye mitandao ya kijamii Bongo, Jacqueline Obedi almaarufu Poshy Queen anasema kuwa, tangu amejifungua mtoto wake wa kwanza, amezidi kuwa mrembo, tofauti na hata alipokuwa hajajifungua.

Akizungumza, Poshy anasema kuwa, watu wengi wanadhani unapopata mtoto, basi mwili unaharibika, lakini ukweli ni kwamba ukizaa na ukajikubali mwili unakuwa mzuri na unaongezeka mvuto.


“Tangu nimejifungua kwa kweli siku hadi siku naona kabisa mvuto umeongezeka sana, maana wengine walikuwa wanasema nikijifungua nitaharibika, lakini ukweli ni kwamba tangu nijifungue nimezidi kuwa bomba sana na
ninavutia tu tofauti hata na mwanzo,” anasema Poshy ambaye ni mama wa mtoto mmoja.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger