4/27/2022

PSG, Real Madrid zampa kiburi PAUL Pogba

 


Kutoka nchini Uingereza inaripotiwa kuwa Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amepokea offa mbili za usajili kutoka klabu ya Real Madrid ya Hisapania na PSG ya Ufaransa. Kiungi huyo atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu pindi mkataba wake utakapomalizika na Manchester United.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa na mshindi wa kombe la Dunia mwaka 2018 mapema hii leo iliripotiwa kuwa amejitoa kwenye kundi la Whatsapp la wachezaji wa Manchester United ambalo wamekuwa wakiwasaliana wachezaji wote. Lakini pia kuwajuza kuwa anaondoka klabu hapo mwishoni mwa msimu huu.

Ripoti mbalimbali kutoka Uingereza hii leo zimeripoti kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hatasaini mkataba mpya wa kuendela kusalia katika viunga vya Old Traford na tayari amepokea offa za usajili kutoka PSG na Reala Madrid ambazo zote zimeonyesha nia yakutaka kumsajili katika dirisha la usajili la majira ya jota.

Kuna uwezekano mkubwa Pogba asionekana tena uwanjani msimu huu, baada ya kocha wa klabu hiyo Ralf Rangning kuthibitisha hilo kufuatia kuwa na majeraha ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpoo mchezo ambao United ilipoteza kwa kunyukwa mabao 4-0.

Pogba alijiunga na Manchester United msimu wa 2016-17 kwa ada ya uhamisho ya pauni million 89 ambayo ni zaidi ya billion 261 kwa pesa za kitanzania (261,108,509,889,365.00) akitokea katika klabu ya Juventus ya chini italia. Na amecheza jumla ya michezo 226 katika michuano yote na amefunga mabao 39 ameshinda makombe mawili akiwa na timu hiyo kutoka jiji la Manchester.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger