Rais mstaafu Honduras Apelekwa Marekani Kwa Tuhuma za Madawa ya Kulevya


 

Rais wa zamani wa Honduras amepelekwa Marekani ili kukabiliwa na madai ya ulanguzi wa madawa ya kulevya, chini ya miezi mitatu tu baada ya muhula wake kukamilika. Juan Orlando Hernandez amekabidhiwa kwa maafisa wa Marekani wa kitengo cha kukabiliana na mihadarati katika uwanja wa ndege ulioko katika mji mkuu Tegucigalpa. 


Hernandez mwenye umri wa miaka 53 mbali na madai ya ulanguzi wa mihadarati atakabaliwa na mashtaka ya kusafirisha silaha Marekani kinyume cha sheria. 


Anadaiwa kusaidia katika ulanguzi wa kilo laki tano za madawa ya kulevya ya cocaine kutoka Honduras hadi Marekani. 


Hernandez anakanusha mashtaka hayo. Anasema walanguzi wa madawa ya kulevya wanaotaka kupokea kifungo cha muda mfupi Marekani ndio waliompangia njama hiyo.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad