Ticker

6/recent/ticker-posts

Rhino King Atamani Kuzichapa Ngumi na Harmonize Ulingoni

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>


Msanii wa muziki Rhino King ameweka wazi kutamani kupigana na msanii mwenzake Harmonize kufuatia kauli ya Harmonize aliyoitoa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Itakumbukwa, @harmonize_tz siku ya Ijumaa alishare video fupi kupitia insta story yake anayoonekana gym akifanya mazoezi makali ya ngumi huku akitaka mtu yeyote mwenye matatizo naye binafsi wakamalizane ulingoni.


Kauli hiyo hiyo yakibabe kutoka kwa Konde Boy imemuibua msanii mwenzake @rhinoking__ ambaye amejipa jina jipya la Tyson Faru akimjibu Harmonize kwamba yupo tayari kwa pambano hilo, atangaze tarehe.

"Ulitangaza nakujigamba kwamba uko fiti na unataka pambano na yeyote kwenye game, niko hapa Tyson Faru, tayari kabisa kwa pambano na wewe kivyovyote. Tangaza tarehe uliemtaka umeshampata no excuses please nishakutamani"- unasomeka ujumbe wa Rhino King kupitia ukurasa wake.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments