4/18/2022

Rick Ross Akubali Michano ya ROSA Ree, Ampatia Bonge la Shavu Marekani

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA

Msanii Rosa Ree amelamba shavu kwenye lebo ya Maybach Music ya rapa Rick Ross

RICK ROSS au The Boss; ni rapa wa kiwango cha Dunia wa Marekani ambaye huenda amevutiwa na kipaji cha rapa wa Tanzania, Rosa Ree kiasi cha kumpa shavu la kumsimamia kwenye lebo yake maarufu ya Maybach Music ambayo kwa sasa ipo tayari kuchukua wasanii wawili wakali wa muziki kutoka barani Afrika.

Rick Ross amewataja wasanii kadhaa ambao tayari amebahatika kuwategea sikio na pengine kati yao yupo atakayeingia kwenye listi ya wasanii atakaofanya nao kazi.

Na kwa kuanzia wakati akitoa taarifa hiyo rasmi kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rick Ross amemtaja rapa mahiri kutoka kwenye muziki wa Bongo Fleva, Rosa Ree pamoja na Kwesta kutoka nchini Afrika ya Kusini.


Rapa wa Marekani na mmilikiwa lebo ya Maybach Music Rick Ross

Rick Ross amekula Pasaka hii kwenye mitaa mbalimbali ya nchini Angola baada ya kuangusha bonge la shoo nchini Nigeria.

Cc; @sifaelpaul

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger