4/13/2022

Ripoti Mfuko wa Bima ya Afya Yaonesha Wanaume 56 Walijifungua


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere amewasilisha ripoti kwa Waandishi wa Habari leo ambapo ameyataja mapungufu ya udhibiti kwenye mfumo wa madai wa Mfuko wa Bima ya Afya ikiwemo madai 56 yanayoonesha Wanaume walipata huduma ya upasuaji (C/S) au huduma za kawaida za kujifungua wakati huduma hizi hutolewa kwa Wanawake, pia Wanachama 444 waliopata huduma ya kuchunguzwa picha kamili ya damu (full blood picture) zaidi ya mara moja kwa siku moja (hadi mara 30) kwenye kituo kimoja.

"Aidha, kuwapo kwa malipo ya madai yaliyorudiwa, pamoja na madai yanayoonesha wanachama wa NHIF waliopokea miwani ya kusomea zaidi ya mara moja wakati utaratibu unaruhusu kutoa miwani mara moja kwa mwaka"

"Udhaifu huu umesababishwa na kukosekana kwa udhibiti katika mfumo wa madai iliyosababisha hasara ya Sh. Milioni 14.41 kwa mfuko"

"Ninapendekeza kwamba Mfuko wa Bima ya Afya: (a) Kurejesha kiasi kilichopotea kutoka kwa watoa huduma za afya husika; na (b) Kuboresha mfumo wa madai wa CMIS ili kuhakikisha kuwa unasaidia maafisa wanaohusika kuangalia uhalali wa madai yaliyowasilishwa"

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger