Sakho Aipa Jeuri Simba leo Dhidi ya Orlando Pirates Kombe la Shirikisho
MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, ameweka wazi kuwa, kikosi hicho kitaibuka na ushindi katika mchezo wao wa leo dhidi ya Orlando Pirates na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

 

Mangungu amesema, kutokana na uwepo wa wachezaji bora kama Pape Sakho na Bernard Morrison ndani ya kikosi chao, wana jeuri ya kufika mbali zaidi katika michuano hiyo.

 

Kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar, leo Jumapili saa 1:00 usiku, Simba watakuwa wenyeji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Mara baada ya mchezo wa leo, Simba wanatarajia kusafiri kwenda Afrika Kusini, kurudiana na Orlando, Aprili 24, mwaka huu, mshindi wa jumla atacheza nusu fainali ya michuano hiyo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mangungu alisema: “Kama uongozi tumekamilisha maandalizi yote kuelekea mchezo huu, na tupo tayari. Benchi la ufundi na wachezaji nao wamekamilisha maandalizi yao, kilichobaki ni kuonesha uwanjani nini tunaweza kukifanya.

 

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tunaamini katika ubora wa kikosi chetu, tuna wachezaji bora na waliothibitisha uwezo wao kama ilivyo kwa Pape Sakho na  Bernard Morrison, tunaamini  tutashinda na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali.”

STORI NA JOEL THOMAS | CHAMPIONI
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad