4/28/2022

Sakho 'Muda wa Kulipa Kisasi Umewadia'

 


Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal na klabu ya Simba SC Pape Ousmane Sakho amesema yupo tayari kwa mchezo wa Jumamosi (April 30), dhidi ya Young Africans.


Simba SC itakua mgeni kwenye mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na Mashabiki wa soka Nchini Tanzania na kwingineko Barani Afrika, huku ikiwa kwenye hatari ya kuutema ubingwa wa Tanzania Bara.


Sakho amesema kama mchezaji amejiandaa vyema pamoja na wachezaji wenzake, na ana uhakika atafanya vizuri kwenye mchezo huo ambao mara nyingi hugubikwa na Presha kubwa kutoka kwa Mashabiki na baadhi ya Viongozi.

Mchezaji huyo amekumbushia mchezo wa Ngao ya Jamii ambao Simba SC ilipoteza dhidi ya Young Africans kwa kufungwa bao 1-0, ambapo alikua sehemu ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.


Amesema muda wa kulipa kisasi umewadia na utakua siku ya Jumamosi, hivyo amewataka mashabiki wa Simba SC kutokua na hafu kuelekea mtanange huo.


“Mimi kama mchezaji nimejiandaa vizuri pamoja na wachezaji wenzangu kuelekea mechi yetu na Young Africans naamini tutafanya vizuri na kupata alama 3”


“Tangu nije Tanzania Nimecheza mechi moja tu ya Derby ni ile ya ngao walitufunga goli moja la mapema ile mechi, Naamini huu sasa ndiyo wakati wa kulipa deni kwa hiyo mashabiki wasihofu hapo kwa Mkapa kitapigwa haswaaaa.” amesema Sakho


Jemedari: Sijamkimbia Haji Manara

Simba SC inakwenda kukutana na Young Africans huku ikiwa na asilimia kubwa ya kuutema ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu, kufuatia kuachwa kwa alama 13 katika msimamo wa Ligi Kuu hadi sasa, huku timu hiyo ikicheza michezo 19.


Young Africans iliyocheza michezo 20 inaongoza msimamo ikiwa na alama 54, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 41, huku Namungo FC ikiwa nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 29 na Azam FC ipo nafasi ya nne kwa kumiliki alama 28.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger