4/06/2022

Sasa Rasmi Nato Yaingilia Vita ya Ukraine, Yatuma Zana Angamizi za Kivita

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


UMOJA wa kujihami wa nchi za magharibi NATO umeingilia vita kati ya Ukraine na Urusi kwa mara ya kwanza tangu vita hiyo ianze February 24.

Nchi ya Jamhuri ya Czech imekuwa ya kwanza kutoka umoja wa NATO kutoa masaada huo wa ana za kivita ambapo umetoa vifaru vya kivita aina ya T-72, BVP-1 pamoja na Mtambo wa kufyatua makombora kutoka ardhini aina ya aina ya Howitzer.

Zana zote hizo zilipakiwa kwenye Treni na na kupitia mpaka wan chi ya Slovakia ambako zinatazamiwa kwenda nchini Ukraine, picha za video zilioneshwa na kituo cha televisheni cha Jamhuri ya Czech.

Kwa muda mrefu NATO imekuwa ikitoa zana za kujilinda, silaha ndogondogo pamoja na misaada ya kibinadamu kwa nchi ya Urusi japo sasa kwa hatua ya Jamhuri ya Czech kutoa msaada huo mkubwa kutaongeza presha kwa mataifa mengine yanayounda umoja wa NATO kutoa misaada ya zana kubwa zaidi za maangamizi


 
Inahofiwa kuwa kwa hatua hiyo Urusi wanaweza kutambua ni kuingiliwa kwa vita yao kitu ambacho Urusi alishatoa onyo kali mapema kabisa wakati vita inaanza

Wadadisi wa masuala ya kisiasa na vita wanadai kuwa hatua iliyochukuliwa na Jamhuri ya Czech imekuja mara baada ya majeshi ya Urusi kushambulia tena miji ya Mariupol na Kharkiv lakini pia matendo ya uhalifu wa kivita yaliyotekelezwa na majeshi ya Urusi ambayo mataifa mengi ya Ulaya yamelaani.

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Czech Jana Cernochova akiongea Bungeni amesema:


“Naweza kuwahakikishia kuwa Jamhuri ya Czech inaisaidia Ukraine kadri iwezavyo na itaendelea kutoa msaada wa zana za kijeshi ndogondogo na zile kubwa.”


        Jamhuri ya Czech imesema itaendelea kutoa misaada ya zana za kivita ndogondogo na kubwa za maangamizi
Nchi ya Slovakia nayo ipo katika mpango wa kutoa msaada kwa Ukraine ikiwa inaungana na Marekania ambao wamekubali kutoa nyongeza ya msaada wa dola milioni 100 kwa Ukraine sambamba na zana za kutungua makombora.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stolteberg amesema jumuiya hiyo inafanya mazungumzo kuona namna ya kuongeza msaada wa zana za kivita kwa majeshi ya Ukraine katika mkutano wao Brussels Ubelgiji.

Kwa upande mwingine, Rais wa Marekani Joe Biden ameagiza majeshi ya Marekani kulinda mipaka upande wa mashariki mwa mataifa yaliyo kwenye umoja wa NATO na kuwa tayari kukabiliana na hatari yoyote kutoaka kwa majeshi ya Urusi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger