4/16/2022

Serengeti Girls yafanya Kweli Burundi Kufuzu Kombe la DuniaTIMU ya soka ya Taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Girls’, jioni hii imeibuka na ushindi wa mabao 0-4 dhidi ya Burundi.

Mchezo huo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia umefanyika Uwanja wa Urukundo Ngozi nchini Burundi.

Mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Clara Luvanga aliyefunga mawili, Neema Paul na Husna Mpanja

Serengeti Girls waliweka kambi Bukoba tangu Aprili 1, ikiwa na wachezaji 24, baada ya hatua ya awali kuitoa Botswana kwa jumla ya mabao 11-0.


Serengeti Girls inayonolewa na Bakari Shime, endapo itafanikiwa kuiondoa Burundi itakutana na mshindi kati ya Cameroon na Zambia na ikivuka itakuwa wamefuzu Kombe la Dunia.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger