Serikali: Minara ya Simu inayowekwa Katika Maeneo ya Wananchi Haina Madhara

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPAWizari ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema kuwa minara ya simu inayowekwa katika maeneo ya wananchi haina madhara yoyote kwani ina viwango vya chini zaidi vya miale, ambavyo vipo chini zaidi ya viwango vya chini vinavyotakiwa.

Ameyasema hayo Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kundo Mathew wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Momba, Condester Sichwale wakati akiomba Serikali kutoa mwongozo kwa kampuni za simu kuhakikisha wanapolipa pango la ardhi kwa mmiliki watoe pia asilimia kwa serikali za mitaa na vijiji ili kuondoa mgongano wa maslahi kwenye jamii.

Akijibu swali hilo Mathew amesema utoaji wa asilimia hutokana na dhana iliyojengeka kuwa minara iliyopo katika maeneo ya wananchi inawaathiri na ndiyo maana wanataka asilimia kama fidia.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad