google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Shaka asema CCM kushika dola kupo palepale | UDAKU SPECIAL

Shaka asema CCM kushika dola kupo palepale

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema lengo la Chama kuendelea kushika Dola liko palepale na kwamba kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni mtaji mkubwa unaorahisisha kazi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Korogwe … (endelea).

Shaka ambaye ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana katika ziara ya kikazi mkoani Tanga amesema hay oleo Jumatatu, tarehe 25 Aprili 2022.

Shaka amesema kazi kubwa inayofanywa na serikali chini ya Rais Samia ni mtaji mkubwa unaokiuza Chama hicho.

“Katika hili tumpongeze sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambayo mafanikio yake ni mtaji mkubwa kwa Chama chetuna umma kwani unaendelea kuimarisha imani yao kwa CCM na serikali yao,” amesema Shaka


 
Amesema Januari, 1977 wakati TANU na ASP zinaungana kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM), wajumbe wake kwa umoja wao waliweka maazimio mengi moja wapo ni Chama kushika hatamu.

“Chama tunachokiunda tunataka kishike barabara hatamu za uongozi wa shughuli zote za umma kwa maslahi ya wafanyakazi na wakulima wa taifa letu; Chama tunachokiunda tunataka kiwe kiungo kati ya Wanamapinduzi wa Tanzania na Wanamapinduzi wenzetu kokote waliko.” Shaka alinukuu azimio hilo.

Aidha, Shaka alisema kwa tafakuri ya azimio hilo, bila ya CCM madhubuti nchi itayumba, kwa kuwa kiongozi bora hawezi kutoka nje ya CCM.


Maelekezo ya ibara ya 5(1) ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2022 yanayotaka CCM kushinda uchaguzi na kuunda dola kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Shaka amesema, ili hayo yote yatimie ni lazima mambo mawili muhimu yafanyike “mosi, kila mwana-CCM atimize wajibu wake katika uimarishaji wa chama na jumuiya zake na pili, uwajibikaji na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ufanyike kwa weledi, ili kuchochea maendeleo, ustawi wa jamii na kuondosha umaskini.

Shaka amewapongeza wanachama na viongozi wote ambao wanatimiza wajibu wao kwa uadilifu na weledi ili kuhakikisha CCM inaendelea kuwa imara na yenye hamasa zaidi kwa umma.

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2022 mkoani humo, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa huo, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi, amesema kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha mwaka mmoja tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani.


 
Amesema miongoni mwa mafanikio makubwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari ambao uliwarahisishia wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza wote waliochaguliwa kujiunga sekondari mwaka huu.

Aidha, amesema Mkoa wa Tanga upo tayari kuwapokea wananchi wanaohamia mkoani humo kutoka hifadhi ya Ngorongoro na kwamba tayari miundombinu muhimu imewekwa katika maeneo wanaohamia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad