Shangilia ya Mayele yatumika kuitisha simba

 Uongozi wa klabu ya Yanga umetumia mitetemo ya mshambuliaji tegemeo Fiston Mayele kuwatisha wapinzani wao Simba ambao April 30 mwaka huu watakutana nao katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Yanga inaongoza ligi ina pointi 51 baada ya kucheza mechi 19 bila kupoteza huku Simba ambao ni mabingwa watetezi wakiwa na pointi 41 baada ya kucheza mechi 19.

Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa uwepo wa mzee wa kutetema pamoja na wachezaji wengine ni salamu kwa wapinzani wao wote wajao ikiwa ni pamoja na wanaofuata,(Simba).

“Ninadhani kwamba kwa sasa burudani inaendelea, walimbeza Fiston Mayele na kusema ni mchezaji wa kawaida sasa kawafunga Azam FC inakuwa zawadi kwa Zakaria Thabit,ambaye alisema ni mchezaji wa kawaida.

“Kasi hii inaendelea hadi kwa wapinzani wetu hao wajao najua wanajua hivyo wajiandae katika hili mambo mazuri yanakuja na sisi tunaendelea na maandalizi,” amesema.Bumbuli.

Zimebaki siku 18 kabla ya Yanga vinara wa ligi wenye pointi 51 kumenyana na Simba, Uwanja wa Mkapa.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad