Ticker

6/recent/ticker-posts

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limemtaka Masoud Kipanya Kupeleka Gari lake

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limemtaka Masoud Kipanya kufika katika Ofisi za TBS na gari la kutumia umeme alilolibuni hivi karibuni ili liweze kukaguliwa na baadaye aweze kupata leseni na cheti cha ubora wa viwango.

Wito huo umetolewa jana Aprili 14,2022 Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Viwango TBS, Yona Afrika wakati walipotembelea karakana ya Masoud Kipanya SIDO ili kuona ubunifu alioufanya kwa kutengeneza gari la kutumia umeme.

“Lengo hasa ni kutaka kuangalia hili gari linakidhi viwango, kwahiyo hatua ya kwanza ambayo tutaifanya kwasababu mpaka tunakuja hapa tuliwasiliana na Masoud Kipanya pindi tu alipotangaza na kutusisitizia ngoja kwanza amalizie matengenezo ili itakapofika kipindi atakapotaka leseni ndio twende kujiridhisha”

Kwa upande wake Masoud Kipanya ameipongeza TBS kwa kazi wanayoifanya hivyo atajitahidi kuafanyia kazi yale yote ambayo ataelekezo na TBS ili kuweza kutimiza malengo yake ambapo amewashauri Wabunifu wengine waliopo mitaani waweze kujitokeza na kufika TBS ili waweze kukaguliwa bidhaa zao ambazo wamebuni na kuweza kutimiza malengo yao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments