Ticker

6/recent/ticker-posts

Silaha Nzito Nzito za Urusi Zimeonekana Zikizunguka Belarus

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>
Kituo cha Telegram cha Belarusi Belaruski Hayun, kinachounga mkono Ukraine kinasema kuwa kimeona harakati kubwa za usafirishaji wa vifaa vya jeshi la Urusi kwa treni kote Belarus siku ya Jumapili.

Inasema treni zilizojaa vifaa vya kijeshi zimeonekana katika vituo vya reli katika mji mkuu Minsk na pia kusini-mashariki mwa Belarus, ikiwa ni pamoja na vituo vya Kalinkavichy, Khoyniki na Homel Kaskazini.

Malori na mizinga pia ilionekana kwenye treni katika kituo cha reli cha Rechytsa kusini mashariki.

Mifumo ya makombora ya kuzuia ndege na magari ya kivita aina ya amphibious yalionekana yakisubiri kupakiwa.


Ndege sita za kivita na ndege za usafiri zilipaa kutoka uwanja wa ndege wa Baranavichy magharibi mwa Belarus na helikopta kadhaa za Urusi zilipaa kutoka Machulishchy karibu na Minsk.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments