4/17/2022

Simba na Pirates..Mechi Yenye Hadhi ya Robo Final
Tumeshudia dakika 90 zenye mchezo wa kimbinu sana kutoka kwa walimu tofauti,. falsafa ya Pablo ni kushambulia ili kupata matokeo na kocha wa Orlando Pirates kuzuia ili kupata sare na kupunguza idadi ya magoli.

Kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo simba walionyesha dhamira ya kutafuta matokeo kwa kutengeneza mashambulizi haraka sana, ila Orlando Pirates walikuwa na kazi ya kuwanyima uhuru simba wa kutengeneza nafasi za kutosha

Eneo la kiungo la simba lilikosa ubunifu zaidi wa kutengeneza nafasi za kutosha na kuwalazimisha Orlando Pirates kufanya makosa,mashambulizi mengi ya simba walianzia pembeni sehemu ambayo Orlando walikuwa imara

Takribani dakika zote Orlando Pirates waliamua kuzuia na kufanya mashambulizi ya kushtukiza mpaka pale walipofungwa goli moja wakaanza kushambulia kutafuta sare it was too late.

Note.

1.Morison anajua namna ya kutafuta nafasi kikubwa

2.Inonga huyu ni mtu na nusu kabisa

3.kwa namna wanavyozuia Orlando Pirates simba ilikuwa ngumu kutengeneza nafasi

4.Dakika 90 za kule South Africa ndio zitaamua nani anaenda nusu final

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger