4/06/2022

Simba si Mwenzetu Ujue...Unaambiwa yakomba Sh3.8 Bilioni CAF

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Simba imevuna pesa hizo zimevunwa kuanzia msimu wa 2018 kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya Simba kuifunga Nkana mabao 3-1 na kutinga hatua ya robo fainali.

Pia msimu uliofuata Simba ilishiriki tena michuano hiyo na kutinga hatua ya robo fainali kwa kumtoa As Vita mabao 4-1.

Simba kutinga hatua hizo mara mbili mfululizo ilivuna Sh 3 bilioni baada ya kupata Sh1.5 bilioni msimu wa 2018 na Sh1.5 bilioni msimu wa 2019.

Kutinga hatua hiyo sasa, Simba wanasubiri bonasi ya Sh 800 milioni kwenye mashindano hayo na kufanya kufikia Sh3.8 bilioni ndani ya miaka minne. Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema; “Kutinga hatua ya robo fainali sio mwisho wa kushiriki bado tuna kazi kubwa ya kuingia kwenye rekodi nyingine. Tunawashukuru Wachezaji kwa ujumla kwa kufikia malengo tunahamia kwenye ligi tunawekeza nguvu.”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger