4/20/2022

Simba yamzulia balaa kocha Orlando Pirates 
LICHA ya dakika 90 za pili za mechi ya marudiano ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika zikisubiriwa kuamua timu itakayotinga nusu fainali kati ya Orlando Pirates na Simba, Jumapili wiki hii,...

Mandla Ncikazi na Fadlu Davids.
...mashabiki wa miamba hiyo ya Afrika Kusini wamecharuka wakitaka Kocha wa ‘Buccaneers’ hao, Mandla Ncikazi na mwenzake, Fadlu Davids, kutimuliwa.

Hatua hiyo, imekuja baada ya Orlando Pirates kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Simba katika mechi ya robo fainali ya kwanza iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Jumapili iliyopita, shukrani kwa Shomari Kapombe aliyefunga bao hilo pekee kwa mkwaju wa penalti dakika ya 67 baada Bernard Morrison kuchezewa madhambi ndani ya eneo la hatari.

Pamoja na Ncikazi kushusha lawama kwa mwamuzi wa mechi hiyo kuwa aliibeba Simba pamoja na shutuma nyingi kwa waamuzi waliokuwa chumba cha VAR, kwamba walizima mtambo kwa lengo la kuwabeba wenyeji, lakini mashabiki wa timu hiyo wametaka atimuliwe na msaidizi wake kutokana na uwezo wao mdogo kiufundi.

Mashabiki wa Orlando Pirates wameutumia mtandao wa kijamii wa klabu hiyo kuelezea mfadhaiko wao kutokana na matokeo hayo wakitaka Ncikazi na kocha mwenzake, Davids kutimuliwa.

 
Hizi hapa ni baadhi ya ujumbe kati ya nyingi zilizotumwa katika mtandao wa klabu hiyo baada tu ya matokeo hayo ya Jumapili:- Tusipoamka na habari kwa ufupi kesho, nitapumzika kushabikia hii Mandla Ncikazi FC, nimechoka kudhalilishwa hivi. #NcikaziLazima Aondoke (@NkarnyiK_88)

Orlando Pirates imekufa. Njia pekee ya kuirejesha ni kuwafukuza wote wawili Mandla na Fadlu. Achia Ndlovu, Mphontshane, Mabaso, Mntambo, Djvukamanje, Dlamini, Pepra, Lepasa na ununue wachezaji wenye ubora. — huwi_freeman (@NMochelete) Aprili 17, 2022

Angalau tumebakiza mechi tano au zaidi kabla ya mwisho wa msimu. Nimemchoka huyu jamaa. Tangu amefika hakuna mabadiliko kabisa ya kuonyesha kuwa kuna mtu mpya mwenye mamlaka!!!— Mogomotsi Mhure (@ TheRealPanyasa) Aprili 17, 2022


@orlandopirates ni wakati wake wa kuwaruhusu wawili hao wa muda kurudi kwenye timu zao ndogo, wamepoteza muda na nafasi zetu vya kutosha. — Lindisipho_Psyfo (@Sipho_Psyfo5) Aprili 17, 2022

Hatuheshimiwi kama mashabiki wa Orlando Pirates. Ncikazi na Fadlu ni makocha wa daraja la kawaida, lazima waende.

Irvin Khoza lazima pia aamue kama bado anataka kuinoa timu hii au la, huu ni upuuzi.— NativeOfGiyani (@Tlangelani87) Aprili 17, 2022

Inaonekana kama timu hii ya ufundi ya Orlando Pirates ina mizozo mingi sana na wachezaji wakubwa, ambao hawafai vya kutosha kwa klabu kubwa.— Boksbrizio (@ Boks_26) April i17, 2022

 
Orlando Pirates inacheza aibu ya takataka. — Dumizulu Ka Nkwanyana (@LaDumezulu) April 17, 2022

#Ncikazi Lazima Aondoke Orlando Pirates wanacheza soka la kutatanisha sana chini ya makocha hawa wawili wa kawaida wasio na uzoefu wa timu kubwa, wanachezesha wachezaji wa kawaida kama Dlamini, Ndlovu, Peprah huku tuna wachezaji kama Mhango, Lorch, Mntambo, [email protected] #Pirates. — Khayelihle (@Khaye_Mabaso) Aprili 17, 2022

Makocha hawa lazima waondoke ili kumaliza kutuletea sifa [email protected].— Engineer Mat┼íhela Koko, MBL (@koko_matshela) Aprili 17, 2022 Mpira wa Ncikazi ndio mbaya zaidi.

Soka la kutisha nililolishuhudia. ‘Subs’ (watokea benchi) walikuwa wabaya zaidi. @orlandopirates— KING XERXES (@MorganBilal) Aprili 17, 2022

Wakati huo huo baadhi ya mashabiki walikataa kumlaumu Ncikazi badala yake wamemuunga mkono kwa kitendo chake cha kukerwa na matumizi ya VAR na kauli yake ya madai kuwa mwamuzi aliisaidia Simba nchini Tanzania. @CAF_Mtandaoni . VAR haina maana barani Afrika.

Timu zinaibiwa mbele ya VAR. Mchezo kati ya Al Ahly dhidi ya Raja Casablanca; Simba Vs Orlando Pirates.

Waamuzi hao hawakuwahi kurekebishwa na VAR licha ya kufanya makosa makubwa— Mashudu Chairman Mundalamo (@Shudulizah2) Aprili 17, 2022

@orlandopirates wamecheza Africa kwa miongo kadhaa, matukio ya nje ya uwanja yanatarajiwa, lakini wakati kuna VAR ungetegemea uwanjani majambazi yatashughulikiwa lakini maafisa walithibitisha kuwa VAR hii itumike tu kuendeleza nia zao na sio kurekebisha. makosa yao https://t.co/ WJpT1aWWaf— Konke Ndaba (@ndabasbonga) Aprili 17, 2022

Kuwa wa kwanza kutoa maoni

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger