Ticker

6/recent/ticker-posts

Steve Nyerere Akerwa na Utani wa Manara, Aamua Kumchana Makavu

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>
Msemaji wa Yanga Haji Manara amekuwa na utani wa muda mrefu na Msanii wa Bongo Muvi Steve Nyerere
STEVE NYERERE au Tivu Ake; ni komediani wa Bongo Movies ambaye ameshindwa kuvumilia masihara ya Semaji la Yanga, Haji Manara na kujikuta akimpa tusi.

Steve ameposti picha ya binti yake mkubwa kisha akaandika; “Tafuta muda wa kukaa na familia, kujifanya upo bize hakusaidii kama familia haikuoni. Rafiki wa kwanza kwenye maisha yako ni familia yako…”

Baada ya hapo, mashabiki wake walianza kutoa maoni mbalimbali huku Manara akiandika; “Chuma changu cha tatu mashallah…”


Msemaji wa Yanga Haji Manara
Kitendo kinaonekana kumkera Steve ambaye amejikuta akimjibu Manara kwa tusi kwa kumuambia; “Achaga ….(tusi) basi kaaaaaa…”


 
Wachangiaji wengine walidai kuwa Steve atakuwa amemaindi baada ya Manara kumtania kuwa atamuoa mwanaye mke wa tatu baada ya hivi karibuni kuoa mke wa pili

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments