TANESCO walivyolipana posho za mabilioni bila kodi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amebaini Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kulipa posho za Sh. bilioni 61.64 kwa wafanyakazi wake pasi na kutoza kodi.

Katika ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka 2020/21 iliyowasilishwa bungeni Jumanne, CAG Charles Kichere anasema amebaini shirika hilo kutotoza kodi ya Sh. bilioni 17.4 kwenye posho za watumishi.

Anafafanua kuwa Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Kodi ya Mapato Sura ya 332 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2019) kinasema mapato ya mtu binafsi kutokana na ajira kwa mwaka wa mapato yatakuwa faida aipatayo mtu huyo kutokana na ajira ya mtu huyo kwa mwaka wa mapato.

Vilevile, CAG anasema Kifungu cha 7(3)(k) cha sheria hiyo kinaeleza kuwa katika kukokotoa faida aipatayo mtu binafsi kutokana na ajira, posho ambazo hazijumuishwi (posho zisizo za kodi) ni posho ya nyumba, posho ya usafiri, posho ya uwajibikaji, posho ya kazi ya ziada, posho ya muda wa ziada, posho ya mazingira magumu na honoraria kwa mtumishi wa serikali au taasisi ambazo zinalipwa kutokana na bajeti ya vyanzo vingine vya mapato, yaani bajeti isiyotokana na ruzuku kutoka serikalini.

"Hata hivyo, nilipopitia makato ya kodi ya mishahara kwa watumishi wa kudumu, watumishi wa mkataba na watumishi wa muda kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021, nilibaini posho za wafanyakazi zenye jumla ya Sh. bilioni 61.64 hazikukatwa kodi (Sh. bilioni 53.57 kwa wafanyakazi wa kudumu na Sh. bilioni 8.07 kwa watumishi wa muda) ambazo ni faida kwa wafanyakazi.


 
"Hali hii ni kinyume cha Sheria ya Kodi ya Mapato kama ilivyoelezwa hapo juu, hivyo kusababisha kutopelekwa kodi ya Sh. bilioni 17.4 katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Sh. bilioni 15.5 kwa wafanyakazi wa kudumu na Sh. bilioni 1.9 kwa wafanyakazi wa muda.

"Hali hii inaweza kusababisha kuongezeka kwa gharama kwa shirika na faini inayoweza kutolewa na TRA kwa kutowasilisha makato ya kodi kwenye posho za wafanyakazi.

"Ninapendekeza TANESCO ihakikishe kuwa posho zote wanazostahili kulipwa watumishi zinatozwa kodi husika kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332, (kama ilivyorekebishwa mwaka 2019)," CAG anasema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad