4/28/2022

Timu ya Man United Yaendelea Kutaabika


Kuelekea mchezo wa 35 kwa Man United kunako EPL msimu huu, orodha ya majeruhi inaongezeka kwenye kikosi cha timu hiyo.

United watakua uwanjani Alhamisi hii kuchuana na Chelsea ndani ya Old Trafford. Kwa hali ilivyo, The Red Devils inawakosa takribani wachezaji 6 wa kikosi cha kwanza. Kocha Ralf athibitisha.

Pogba, Maguire, Sancho, Shaw, Fred na Cavani wote watakosekana kwenye mchezo huu wakati ambao, Wan Bissaka huenda akakosekana na hivyo orodha kuongezeka zaidi. Hili ni pigo kwa Rangnick ambaye anatoka kwenye vipigo vitatu kwenye michezo 4 iliyopita, anakwenda kuchuana na The Blues.

Kutokana na idadi ya majeruhi kwasasa kwenye kikosi cha Man United, Ralf Rangnick amethibitisha kuwepo na wachezaji 14 tu (pamoja na chipukizi) kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Chelsea hali ambayo inampa mashaka kuelekea mwishoni mwa msimu.

✍️: @omaryramsey

#SNSSports⚽⚽

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger