4/11/2022

Urusi Yapata Tabu Sana..Majeshi ya Ukraine Yatungua Ndege ya Urusi, Yatuma Salamu za Shukrani UingerezaKATIKA hali ya kufurahishwa na maendeleo ya vita yao dhidi ya majeshi ya Urusi Yuriy Kochevenko moja ya wanajeshi wa Ukraine waliotungua Ndege isiyo na Rubani ya Urusi alifurahia tukio hilo kwa kuonesha alama ya kidole na kutuma salamu za shukrani kwa serikali ya Uingereza kutokana na msaada wa zana za kivita walizowapatia ili kukabiliana na mashambulizi ya majeshi ya Urusi.

Mbali na kuwashukuru kamanda huyo aliandika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii akisema watatumia vema silaha zote wanazopewa kama msaada na mataifa mengine.

Uingereza imekuwa ikitoa misaada ya zana za kivita, kuwapa mafunzo askari wa Ukraine pamoja na kuwapatia zana za kujilinda.

Kochevenko alisema:

“Zana za ulinzi wa anga zimesambaratisha drone ya Urusi haya ni mafanikio makubwa kwetu katika kutumia zana hizi kubwa, na hizi ni salamu zetu za shukrani kwa Boris Johnson,”


“Tunaishukuru Uingereza, tunatumia vizuri misaada ya washirika wetu tumeni ya kutosha kwa ajili ya uhuru wetu na wenu pia.”

Picha za drone iliyoshambuliwa zimeonekana katika eneo la tukio huku zikionesha namna zilivyotengenezwa mahususi kwa kuchukua picha na kufanya uchunguzi wa eneo hilo kwa muda mrefu.


                  Ndege ya Urusi imesambaratishwa na makombora ya Ukraine
Mkuu wa Majeshi wa Ukraine kupitia ukurasa wa mandao wake wa Facebook aliandika kuwa Aprili 10 wanajeshi wa Ukraine walitungua Ndege isiyo na Rubani ya Urusi aina ya Orlan-10 kwa kutumia mfumo wa makombora aina ya StarStreak.

Kuangushwa kwa Ndege isiyo na Rubani kunafuatia kauli ya Boris Johnson Waziri Mkuu wa Uingereza ambaye hivi karibui amenukuliwa akisema Uingereza itatoa msaada mwingine wa Zaidi ya Paundi milioni 100 na utafanya kazi kuhakikisha unatoa msaada wa vifaru vingine vya kutosha kwa majeshi ya Ukraine ili kukabiliana na majeshi ya Urusi.

Mauaji ya Kutisha ya raia katika mji wa Bucha yamelaaniwa na mataifa mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yanaiunga mkono Ukraine katika harakati zake za kupambana na majeshi ya Urusi.

Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alifanya ziara ya kushtukiza nchini Ukraine katika mji mkuu wa Kyiv ambapo amenukuliwa akisema kuwa ni vema nchi washirika watoe zana zinazoweza kutumika hasa na wanajeshi wa Ukraine na pia anaunga mkono katika dhana ya kutumia silaha za kujilinda kuliko za maangamizi.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger