Vipande vya Mwanamume Aliyechemshwa Hadi Kufariki katika Kampuni Moja Mjini Thika Kuzikwa KisumuMwanamume aliyepondwa na kuchemshwa hadi kufa katika tanuri ya kampuni moja mjini Thika atazikwa Aprili 9 katika Kaunti ya Kisumu
Glavu zake zilikwama kwenye vyuma, akavutwa na mashine hiyo hadi kwenye tanuri, kupondwa na kuchemshwa hadi kuaga dunia
Polisi walisema kuwa suala hilo litashughulikiwa tu kama kisa cha kawaida cha ajali za kazini
Caleb Otieno, mwanamume aliyepondwa na kuchemshwa hadi kufa katika tanuri ya kampuni ya Blue Nile Rolling Mills mjini Thika atazikwa nyumbani kwao eneo la Kogony katika Kaunti ya Kisumu mnano Jumamosi, Aprili 9.

Vipande vya Mwanamume Aliyechemshwa Hadi Kufariki katika Kampuni Moja Mjini Thika Kuzikwa Kisumu
Mabaki ya Caleb Otieno yatazikwa Jumamosi nyumbani kwao katika Kaunti ya Kisumu. Picha: Moses Ngige.
Mabaki ya mwili wake yaliondoka katika hifadhi moja ya maiti mjini Thika mnamo Ijumaa na kusafirishwa hadi nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi.

Otieno alikuwa na kibarua cha kuweka vipande vya chuma katika moto mkali na siku ya kufa kwake mnano Machi 25, alikuwa kazini kama kawaida.

Inaarifiwa dakika chache kabla ya kifo chake, alimpa mwenzake KSh 50 ili amnunulie chakula cha mchana.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad