4/28/2022

Umaarufu wa Mwanamuziki TEMS Wazidi Kupanda, Apewa Shavu na Mwanamuziki Future wa Marekani


September 2021, mwanamuziki wa kike tokea Nigeria, @temsbaby alipata bahati ya kuwa moja ya wasanii walio shiriki kwenye albamu ya Rapper @champagnepapi inayoitwa Certified Lover Boy.

Bahati hii inarejea tena mwaka huu baada kuwa moja ya wasanii walioshirikishwa kwenye Albamu ya Rapper @future inayoitwa “I never Liked You” inayo tarajiwa kutoka ijumaa hii ya tarehe 29 April, Tems ameshirikishwa kwenye wimbo No.7 pamoja na Drake unaoitwa “Wait For You”

Tems anakuwa ni miongoni mwa wasanii wa Nigeria wanaokuja kwa kasi kwenye ramani ya muziki duniani,na hii ni baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye wimbo wa Essence alio shirikishwa na @wizkidayo

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger