Warembo 3 Pacha Watarajia Kuolewa na Mwanaume MmojaWanawake watatu pacha wa nchini Kenya wanaofanana sana, wamesema kwa sasa wanachumbiwa na mwanaume mmoja ambaye kila mmoja alimpenda kwa nyakati tofauti na wanatarajia kuolewa na mwanaume huyo hivi karibuni.

Cate, Eve na Mary wamesema kuwa katika uhusiano na mpenzi wao haikuwa jambo gumu kwa vile wao ni dada wa karibu na kaika undugu wao wamekuwa wakigawana kila kitu tangu umri wao mdogo.

Wameeleza kuwa Cate ndiye alikuwa wa kwanza kukutana na mwanamume huyo na kuwafahamisha wenzake ambao pia walimpenda ingawa Mary alikiri ndiye anampenda sana mwanamume huyo.


Cate, Eve na Mary wakiwa na Mume wao mtarajiwa
“Nilimwona na kumwambia Mary juu yake kabla ya Eve pia kujua juu yake na kumpenda. Tunapanga kuoana nae na yuko tayari kwa hilo pia,” Cate alisema.


“Tukiwa wadogo mama alike kitufunga kamba nyekundu, kijani, na njano ili kujua ni nani amekula na nani bado hajala, na nhadio sasa kwa ukubwa huu bado baba yeti hajui nani ni nan,” alisema mmoja wa pacha hao.

Kulingana na pacha hao, mpenzi wao hukutana nao kibinafsi Jumatatu, Jumanne na Jumatano kabla ya tarehe ya pamoja ya chakula cha jioni Ijumaa.

Hivi karibuni walitokea pacha watatu wa nchini DRC ambao pia waliolewa na mwanaume mmoja na wakawa na vacati wa Furaha kwa kufanikiwa kuishi pamoja hii ni kutokana na familia nyingi zilizo na watoto pacha, kuwalea wakifanya kila kitu pamoja kutoka kwa umri mdogo hadi mahali ambapo kuchagua kugawana mume kutokuwa jambo ngumu kwao.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad