4/17/2022

Watanzania Walio Kasirika Diamond Kukosa Tuzo Wanapingana na Kauli yakeBaada ya msanii Diamond Platnumz kutoa kauli kuwa Tuzo za muziki Tanzania zilikufa kwasababu yake,baada ya kutopewa tuzo aliyo stahili kupata hadi kupelekea watanzania kuchukia na wadhamini kujitoa kwenye tuzo hizo, kauli hiyo imeleta mabishano makubwa kwenye mitandao ya kijamii na asilimia kubwa ya watu wakipingana na kauli ya msanii huyo.


Kuna wanaoamini kuwa kwa kauli yake,Diamond Ni chui mwenye ngozi ya kondoo,ikiwa na maana kuwa huwa anaonyesha kuwa vizuri na wasanii wenzie kwa nje ila ukweli ni kuwa hana love nao,, lakini kuna wachache wanao amini alicho kiongea ni ukweli wake na kafanya la maana kuliko angebaki nalo moyoni lakini bado hawaiafiki kauli yake kuwa chanzo cha tuzo kufa ni yeye.


Binafsi naona yeye kama Role Model wa wengi, awe na chaguzi ya vitu vya kuongea, na sio kuongea ili mradi kaongea, Maneno yake hayana taswira nzuri hata kidogo kwa serikali na hata tasnia na pia ni tuhuma zisizo na ushahidi.


Nini Maoni yako? Bado natafuta wale watanzania aliosema walimaind kipindi anakosa tuzo

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger