4/09/2022

Watoto Wanane wa Shule Moja Walawitiwa, Hofu yatandaSongea. Watoto wanane wa Shule ya Msingi Tembo Mashujaa, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanadaiwa kubakwa na kulawitiwa kwa nyakati tofauti na kijana ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi.

Kati ya watoto hao, wanane ni wa kiume na mmoja wa kike ambao wana umri kati ya miaka minne hadi tisa.

Pamoja na kufanyiwa vitendo hivyo, inadaiwa watoto hao kufundishwa kufanya vitendo hivyo kwa watoto wenzao na kuwekeana vitu visivyofaa sehemu za siri, ikiwa ni pamoja na kutembea na mafuta ya mgando kwa ajili ya kufanyia kitendo hilo.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wazazi wa watoto hao walisema Machi 21 mwaka huu aligundulika mtoto mmoja wa darasa la kwanza katika shule hiyo kutokana na kuomba ruhusa mara kwa mara kwenda chooni, mwalimu alipomhoji alisema anaharisha na anapata maumivu njia ya haja kubwa.


Mmoja wa wazazi wa watoto, Devotha Mgunya (si jina halisi) alisema walipigiwa simu na uongozi wa kamati ya shule na walipokwenda walielezwa tatizo lililowakuta watoto wao.

“Mtoto mmoja alipogundulika kuwa amefanyiwa kile kitu, alisema hayupo peke yake, kuna wenzake, akaanza kuwataja ambao wote wanasoma darasa moja. Walipohojiwa walikiri kufanyiwa vitendo hivyo na kijana ambaye yupo mtaani,” alisema.

Mtoto mwingine alimweleza mwandishi wa gazeti hili kuwa kutokana na kufanyiwa vitendo hivyo amekuwa akipata maumivu makali anapokwenda kujisaidia, lakini hakusema kwa kuwa alitishiwa kuuawa iwapo atamtaja ‘uncle’ anayewafanyia vitendo hivyo.


Alisema kijana anayedaiwa kuwafanyia vitendo hivyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20, alikuwa akiwadanganya kwa kuwapatia vindege, pipi na kucheza nao kwa kukimbizana. Mmoja wa wazazi, Paulo Joseph (si jina lake halisi) jana walikwenda kituo cha polisi kuchukuliwa maelezo na polisi waliwataka wazazi wengine ambao watoto wao walifanyiwa ukatili huo waende kutoa maelezo yao na Jumamosi waende na watoto kituoni kuhojiwa.

Aliiomba Serikali iwasaidie kwa kuwa watoto wao wameathirika kisaikolojia, kwani wengine wana vidonda sehemu za siri na wanatembea kwa shida.

Mwenyekiti wa kamati ya shule, Paul Joseph alipohojiwa alikiri kuwapo watoto wanane wanaodaiwa kulawitiwa na kwamba mtoto mmoja aliwataja wenzake. “Nilitafutwa ili kufanya kikao cha kujadili jambo hilo, hivyo tuliwaita wazazi wote na kuwahoji na kila mmoja anamtaja mtuhumiwa huyo huyo,” alisema.

Alisema mtoto mmoja alisema aliingiliwa siku hiyo (Machi 21), hivyo kamati ya shule ilimwita mwenyekiti wa mtaa wa Kuchile wanakoishi watoto hao na kumweleza tatizo la watoto hao na kumkabidhi jukumu hilo alishughulikie kisheria.

Alisema katika kikao hicho pia alimuitwa mama wa kijana anayetuhumiwa kuwabaka na kuwalawiti watoto hao na kwamba aliposikia tuhuma zinamhusu mwanawe aliinuka kwenda pembeni kupiga simu, alisikika akitoa maelekezo ya kumtorosha mtuhumiwa.

Mtoto mmoja wa kiume aliyefanyiwa ukatili huo alisema kijana huyo alimtisha kwamba angesema angemchoma kisu.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk Mgafu Majura alipozungumza na Mwananchi alisema taarifa za watoto hao zipo mamlaka ya juu na kumtaka mwandishi awaulize polisi, kwani wanaendelea na taratibu

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger