4/10/2022

Watoto Wawili Wauawa, Watelekezwa BarabaraniKamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Robert Kakwesi
Tabora. Watoto wawili wameuawa na miili yao kutekekezwa pembeni ya barabara Kuu iendayo Kigoma eneo la kata ya Malolo katika Manispaa ya Tabora.

Miili ya watoto hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 14 na 17 imekutwa na alama za kukatwa na kitu chenye ncha kali kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo kichwani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa atatoa taarifa ya awali kesho.

Diwani wa kata ya Malolo ambako miili imekutwa leo Jumamosi Aprili 9, 2022, Zinduna Kambangwa amedai kuwa huenda hao walienda kuiba mahali na ndipo walipopigwa na kitu chenye ncha kali.


"Kama unaenda kwa mtu usiku wa manane sio kwa ndugu yao na kuvunja huo ni wizi ingawa hatutaki watu kujichukulia sheria mkononi"Amesema

Ameeleza kuwa wamefuatilia na kugundua sehemu ambayo huenda ndio walipigwa kutokana na kufuatilia michirizi ya damu.

Amesisitiza kuwa sio jambo zuri na wala haipendezi kwa watu kuuawa kama ilivyokuwa kwa vijana hao na Kisha miili Yao kutelekezwa.

Mkazi wa Malolo aliyeomba hifadhi ya jina lake amedai kuwa vijana hao walienda kuiba katika moja ya nyumba za eneo la Malolo na ndipo walipogundulika na kuuawa na miili yao kuingizwa kwenye mtaro pembeni ya barabara Kuu iendayo Kigoma kupitia Urambo

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger