Waziri Bashungwa Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Morogoro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Hassani Njama Hassani kuanzia leo tarehe 20.04.2022 ili kupisha uchunguzi.

Wakati wa ziara hiyo Waziri Bashungwa alibaini upotevu wa Fedha za miradi na matumizi yasiyo sahihi ya kiasi cha shilingi milioni 231.84 katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Moringe Sokoine zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula, jiko na bweni na kumuagiza Mkurugenzi huyo kuwachukulia hatua za kiutumishi Wakuu wote wa Idara na watumishi waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi katika mradi huo.

Hadi kufikia leo hii hakuna Mkuu wa Idara yeyote ama Mtumishi aliyechukuliwa hatua kufuatia maagizo hayo, aidha Waziri Bashungwa ameendelea kuwataka Wakurugenzi wa Halmashuri zote nchini kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu na kuchukua hatua za haraka pale wanapobaini ubadhifu wa fedha za umma
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad