Wema Sepetu Awafukuza Uwoya na Lulu Nyumbani kwake

 


Mwanadada Wema Sepetu anadaiwa kuwafukuza nyumbani kwake wasanii wenzake Irene Uwoya pamoja na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambao inadaiwa walifika nyumbani kwa nyota huyo kutafuta suluhu ya msuguano uliopo baina yao.


Taarifa za awali zinasema kuwa Irene Uwoya na Lulu walifika nyumbani kwa Wema Sepetu wakiwa na wasanii wenzao ambao ni Aunt Ezekiel, Jackline Wolper pamoja na Kajala ambao walikwenda kama wasuluhishi.


Pampja nao waliwashirikisha viongozi wa wasanii hao (managers) ambaye ni Martin Kadinda pamoja na Aloy.


Inaelezwa kuwa kwa kipindi kirefu Wema na Lulu wamekuwa hawana maelewano mazuri kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi huku kwa upande wa Irene Uwoya suala la kashfa zilizotolewa na mpambe wake “Aristoste’ dhidi ya Wema zikitajwa kama moja ya sababu iliyosababisha kukosekana kwa maelewano baina yao.


Mpaka sasa bado taarifa za ndani zaidi kuhusu marumbano ya nyota hao hazijawekwa wazi licha ya kuenea kwa video inayoonesha sehemu ya mazungumzo mpaka hatua za kuzuka kwa mgogoro huo uliopo.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad